Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018

In Kitaifa
  Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata elimu ya mpiga kura, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, baada ya Serikali kutenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kazi hiyo katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhani kwa nyakati tofauti, wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika vituo vya redio vilivyoko mkoani Dodoma.
Amesema kuwa maandalizi ya uboreshaji huo ni pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura, kupitia vituo vya redio nchi nzima mpango ambao umeanza kutekelezwa, kwa baadhi ya mikoa nchini.
Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa kipindi hicho Tume itatoa kadi mpya ya mpiga kura kwa watakaoandikishwa upya, waliopoteza kadi na kadi zilizoharibika, kwa wanaohamisha taarifa zao ikiwemo waliohamia Dodoma, na kufuta wapiga kura waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Wazazi wahimizwa kuzingatia Elimu Mbeya.

Afisa Tarafa wa Sisimba John Mboya amewataka wazazi na walezi kata ya Itagano Jijini Mbeya kuzingatia suala la elimu

Read More...

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu