Tume ya Uchaguzi na viongozi wa upinzani wakubaliana kuhusu kituo cha kujumuisha matokeo.

In Kimataifa

Muungano wa upinzani nchini Kenya NASA, umeafikiana na Tume ya Uchaguzi IEBC kuhusu utaratibu wa upinzani kuwa na kituo chao cha kujumuisha matokeo ya urais wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

Baada ya kukutana na viongozi wa Tume ya Uchaguzi jijini Nairobi, imekubaliwa kuwa upinzani unaweza kuendelea na mpango wao wa kuwa na kituo cha kujumuisha matokeo lakini usitangaze matokeo.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati, amesema mawakala wa upinzani watakuwa na haki ya kisheria  kupata matokeo yote ya mwisho kutoka katika vituo mbalimbali lakini akasisitiza kuwa ni Tume tu ndiyo itakayokuwa na mamlaka  ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Mwafaka huu unamaanisha kuwa, tofauti zilizokuwepo kati ya pande hizi  mbili zimetatuliwa na suluhu kupatikana.

Kigogo wa upinzani Raila Odinga na mwenzake Kalonzo Musyoka wamekuwa wakisisitiza kuwa upinzani umeweka mikakati ya kuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo na kuyatangaza na kusisitiza kuwa hakuna atakayewazuia kufanya hivyo.

Muungano wa NASA hivi karibuni umekuwa ukihoji utayari wa Tume ya Uchaguzi nchini humo na hata kusema hauwaamini Makamishena hao.

Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi inasema zoezi hilo litakuwa huru na haki na ipo tayari kuandaa Uchaguzi huo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu