Twaweza watoa utafiti juu ya huduma za afya nchini

In Afya, Kitaifa

Kuna dalili za kupungua muda wa wagonjwa kumuona daktari, baada ya utafiti kuonyesha wale waliokuwa wakisubiri kwa zaidi ya saa moja idadi yao imeshuka kwa asilimia tano, ndani ya miaka mitatu iliyopita.

Utafiti mpya wa asasi ya kiraia ya Twaweza uliozinduliwa leo, unabainisha idadi ya wananchi wanaosubiri kumuona daktari kwa zaidi ya saa moja, imeshuka kutoka asilimia 25 mwaka 2014 hadi asilimia 20 mwaka huu.

Hii ina maana kuwa kwa sasa ni mtu mmoja kati ya watu watano wanaoenda kituo cha afya, ndio husubiri zaidi ya saa moja kupata huduma kulinganisha na mtu mmoja kati ya wanne miaka mitatu iliyopita.

Mbali na mafanikio hayo utafiti huo wa toleo la 19 la Sauti za Wananchi, unabainisha kuwa wananchi sita kati ya 10 sawa na asilimia 61, wanapata huduma za afya katika vituo vya afya vya Serikali, kiwango ambacho ni sawa na cha mwaka jana.

Mwaka 2014 idadi ya wananchi waliokuwa wakipata huduma za afya kwenye vituo vya umma, ilikuwa ni takriban watano kwa kila 10 sawa na asilimia 45.

Kutokana nay ale yalimo katika utafiti huo  mbunge wa kigoma mjini Zitto kabwe, akiongelea utafiti huo na kusema kuna umuhimu kwa kila mtanzania kuwa na bima ya afya.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu