Nchini Kenya mjadala unaendelea kufuatia kiongozi wa upinzani Raila Odinga kujiondoa, katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26.
Kumekuwa na maswali mengi kuhusu je uchaguzi utafanyika au mgombea aliyebaki Rais Uhuru Kenyatta, atangazwe kuwa mshindi bila kufanyika uchaguzi.
Tayari Rais Uhuru Kenyatta amesema pamoja na kujiondoa Raila Odinga wa NASA uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa.
Katika kupata ufafanuzi zaidi kuhusu utata huo Antenna imemnasa Mwandishi wetu Dkt Alutalala Mukhwana, ambaye ni mwanasheria aliyebobea katika masuala ya Kikatiba nchini humo.
Kwa upande wake Rais uhuru Kenyeta hakukaa kimya baada ya Raila Odinga kutangaza kujitoa katika uchaguzi huo, ni lipi alilolisema msikie hapa.
Hata hivyo habari nyingine ni kwamba, mahakama Kuu nchini humo imeamuru mgombea urais wa chama cha Thirdway Alliance Ekuru Aukot, aliyekuwa ameshiriki uchaguzi mkuu tarehe 8 Agosti, ashirikishwe kwenye uchaguzi mkuu mpya unaopangiwa kufanyika tarehe 26 Oktoba.
