#UEFAChampionsLeague: Klabu za EPL na La Liga zatawala 16 bora

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hatua ya makundi imemalizika jana ambapo tayari timu 16 kati ya 32 zimefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora, hatua ya mtoano.

Kwenye hatua hiyo klabu za kutoka Ligi Kuu Uingereza  na zile kutoka La Liga ndio zimetawala 16 bora ya michuano hiyo, ambapo Uingereza imeingiza timu zote tano huku Hispania ikifanikiwa kuingiza timu tatu.

Timu zilizofanikiwa kupita kutoka Uingereza ni Liverpool, Manchester United, Manchester City, Tottenham Hotspurs na Chelsea.

Na timu zilizofuzu kutoka Uhispania ni Real Madrid, Barcelona na Sevilla huku klabu ya Atletico Madrid ikitolewa mapema kwenye michuano hiyo.

Kwa upande mwingine timu 16 ambazo  zimetolewa kwenye michuano hiyo zitaingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Europa.

Droo ya kutangaza ratiba ya hatua ya 16 bora ya kombe la klabu bingwa barani Ulaya itafanyika jumatatu ya tarehe 11 Desemba 2017, huko mjini Nyon , Uswizi.

Exit mobile version