UHAKIKI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA UGANDA KUFANYIKA UHOLANZI

In Kimataifa

Taarifa kutoka nchini Uganda zinasema daftari la kitaifa la wapiga kura limepelekwa Uholanzi kwa ajili ya kuhakikiwa.

Tume ya uchaguzi imeipa zabuni kampuni ya Uholanzi kuondoa majina ya watu walioandikishwa zaidi ya mara moja wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Januari.

“Tumeanza mchakato wa kuwathibitisha wapiga kura ili kuhakikisha kuwa wapiga kura wanaostahili tu wanaonekana kwenye daftari na kwamba watapiga kura mara moja,” msemaji wa tume hiyo Paul Bukenya amenukuliwa akisema.

Haijulikani kama vyama vya siasa vilijulishwa kuhusu hatua hiyo.

Raia wa Uganda watapiga kura kuchagua rais na wabunge tarehe 14 mwezi Januari. Wagombea 11- akiwemo Rais Yoweri Museveni- watawania nafasi hiyo ya juu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu