Ujerumani yaondoa tahadhari ya usafiri kwa mataifa mengi ulaya

In Kimataifa

Ujerumani imeondoa tahadhari za usafiri kimataifa ilizoweka kwa mataifa mengi ya Ulaya miezi mitatu iliyopita kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya Ujerumani, imeondoa masharti hayo ya usafiri kwa mataifa 27 ya Ulaya kuanzia usiku wa kuamkia leo.

Ujerumani pia inatarajiwa kusitisha vizuizi vyake katika mipaka yake kuanzia leo.

Hatua hiyo inaenda sambamba na pendekezo la kamisheni ya Umoja wa Ulaya linalozimihimza nchi wanachama kufungua mipaka kuanzia wiki hii.

Hata hivyo raia wa Ujerumani bado wanashauriwa kuepukana na safari ambazo si za lazima nje ya nchi ambazo tahadhari hazijaondolewa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Saba washikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya hakimu.

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watu saba kwamauaji ya Hakimu Mkazi wa wilaya ya Handeni mkoani TangaJoachim Mwakyolo

Read More...

Ali Reza Akbari ahukumiwa kifo

Iran imemuhukumu kifo afisa mkuu wa zamani wa ulinzi baada kumkuta na hatia kwa mashtaka ya kuifanyia ujasusi Uingereza,

Read More...

Polisi wakamata usafiri uliotumika kuutupa mwili Chiloba

Miongoni mwa waliokamatwa ni watoto wawili huku mshukiwa mkuuJackton Odhiambo akikiri kumuua mwanamitindo huyo kwa usaidizi wawashirika wawili ambao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu