Umoja wa Mataifa umegundua Umoja wa makaburi zaidi ya 38 katika jimbo la kati la Kasai.

Umoja wa Mataifa umegundua kile kinachoonekana kuwa ni makaburi zaidi ya pamoja 38 katika jimbo la kati la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linalokumbwa na machafuko la Kasai.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Pamoja ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Congo Jose Maria Aranaz amewaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa makaburi hayo mapya 38 yanajumuisha 31 katika eneo la Diboko, na saba katika eneo la Sumbula, upande wa magharibi mwa Kasai.

Yaligunduliwa kufuatia uchunguzi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na idara ya mahakama ya jeshi la Congo kati ya Julai 4 na 7.

Ugunduzi huo unafikisha 90, jumla ya makaburi ya pamoja yaliyotangazwa na Umoja wa Mataifa au maafisa wa Congo katika mkoa huo.

Mzozo wa Kasai ulichochewa na kukataa kwa serikali kumpa utambulisho rasmi Jean-Pierre Mpandi, anayefahamika kama Kamuina Nsapu, kuwa mmoja wa viongozi wa kitamaduni wa eneo hilo.

Mpandi kisha akawatumia wapiganaji wake kuanzisha uasi dhidi ya uwepo wa serikali katika eneo hilo.

Exit mobile version