UN: Mashambilizi 17 yamefanywa katika vituo vya afya nchini Libya

Mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa nchini Libya imesema matukio 17 ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya yamerekodiwa katika mji wa Tripoli na viunga vyake, eneo ambalo kumeshuhudiwa mapigano ambayo yamekuwa yakisababisha mauwaji kwa zaidi ya mwaka sasa. Mbabe wa kivita Khalifa Haftar, anadhibiti eneo kubwa la mashariki mwa Libya na Aprili mwaka uliopita kuanzisha mashambulizi ya kuudhibiti mji wa Tripoli, ambao ni makao makuu ya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa. Serikali hiyo inawabebesha lawama ya mashambulizi hayo majeshi tiifu kwa Haftar, lakini msemaji wa wapiganaji hao amekanusha kuhusika.

Exit mobile version