EEEEH bhana kama una kumbukumbu nzuri nishakupa taarifa za T.I kuachana na mkewe Tiny ambaye wamekuwa pamoja kwenye ndoa miaka 6 na kuachana December mwaka jana 2016.

Sasa baada ya T.I kuachana na mama toto wake alihamishia penzi lake kwa Video Queen maarufu ajulikanaye kama Bernice Burgos ambaye alihusika kama model kwenye Video ya DjKaled Do you mind ambayo amemshirikisha Chris Brown, Nicki Minaj, August Alsina, Jeremih Future na Rick Ross
Sasa kuna taarifa kwamba Msanii wa Nigeria Oladapo Daniel Oyebanjo maarufu kama D’banj naye anakula Mrembo huyo.

Taarifa hizo zimeongezwa na nguvu na Uwepo wa DBanj na Mrembo huyo kwenye bata la pamoja huko katika visiwa vya Bahamas kaskazini mwa Kuba

Kupitia mtandao wa Snapchat model huyo alitupia picha akiwa ameshikwa kiuno na D’banj.
Ila pamoja na minong’ono hiyo kwamba wanakwich DBanj na Model huyo kwa upande wa DBanj yeye anasema wanafanya Video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Be With You’ ambao Bernice ametumika kama model.
DBanj anayemiliki DB Records amesema ataendelea kufanya kazi na watu wenye viwango vya Kimataifa kwa ajili ya kuhakikisha Kazi zake zinafika anapotaka.
MREMBO HUYO ALIKULA SHAVU KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI
BAADHI YA PICHA ZA MREMBO HUYO
