UNHCR wazindua mpango mpya wa mambo ya Fedha Rwanda

In Kimataifa

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa mataifa UNHCR kwa kushirikiana na serikali ya Rwanda, wamezindua mpango mpya wenye lengo la kuwashirikisha wakimbizi kwenye mambo ya fedha.

Mpango huo uliozinduliwa siku moja kabla ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya wakimbizi, unatarajiwa kuwawezesha wakimbizi kujitegemea kiuchumi kwa kutumia miradi ya kujipatia fedha, kupitia misaada na mikopo.

Waziri wa Rwanda anayeshughulikia usimamizi wa Majanga na Wakimbizi Seraphine Mukan tabana, amesema fedha hizo zitatolewa kwa mfuko wa mzunguko.

Mwakilishi wa UNHCR nchini Rwanda Bw Saber Azam amesema hatua hiyo ya Rwanda ,inafuatia ahadi iliyotolewa na serikali ya Rwanda kwenye mkutano wa kilele uliofanyika mjini New York, kwamba itaruhusu wakimbizi kuwa sehemu ya maendeleo ya uchumi na jamii.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

CCM waongeza nafasi za Wajumbe Halmashauri kuu

Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu amesema ili kupanua wigo, halmashauri kuu

Read More...

Washukiwa 25 wanaodaiwa kupanga njama za mapinduzi wakamatwa Ujerumani

Maelfu ya polisi leo wamefanya msururu wa misako kote Ujerumani wa washukiwa wa siasa kali za mrengo wa kulia

Read More...

Mkuu mpya wa chuo cha Arusha asimikwa.

Chuo kikuu cha Arusha kimemsimika mkuu mpya wa chuohicho wakati wa mahafali ya 16 ambayo yamefanyika chuonihapo.  Mkuu aliyeachia nafasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu