Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwa jina la Dkt. Abdallah Juma.

In Kitaifa
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umemtia mbaroni kijana mmoja aliyekuwa akijifanya daktari na alikuwa akijitambulisha kwa wagonjwa kwa jina la Dkt. Abdallah Juma.
Aidha, kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu ya Hospitali hiyo huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kshtukiwa na kukamatwa.
Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo.
Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema hospitali imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na wahalifu wakiwamo watu wanaojiita ni madaktari kama huyo ambaye amekamatwa leo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Trump apiga marufuku raia wa mataifa 12 kuingia Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini tangazo jipya linaloweka marufuku kali kwa raia wa mataifa 12 kuingia nchini

Read More...

Serikali Yafuta Usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Linaloongozwa na Askofu Gwajima

Serikali kupitia Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa, imetangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na

Read More...

KATIBA YA CCM YAFANYIWA MABADILIKO 

Kwa mujibu wa taarifa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu