Uongozi na wanafunzi wa shule za msingi ukombozi na Ongosengiu zilizopo kata ya sinoni mkoani Arusha, zimeishukuru halmashauri ya jiji kwa kuweza kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabili, kwa mda mrefu katika shule hizo
Wakizungumza baada ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ,katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kutatua kero zinazowakabili wananchi baadhi ya waalimu wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya vyoo, na madarasa hali ambayo inawapelekea kuwa na wasiwasi wa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekabithi jumla ya madarasa 17 ,katika shule hizo huku akiahidi kujenga vyoo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili waalimu wa shule hizo
Hata hivyo amewataka waalimu wa shule za msingi na sekondari kufanya kazi kwa ufanisi ,ikiwa ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi kwa bidii ili kuweza kujenga Tanzania ya viwanda ambayo Ndio azma ya Seriakali ya Awamu ya Tano .
