Upo uwezekano wa wanyama kama mbwa mwitu, tembo, sokwe na faru mweusi kutoweka.

In Kitaifa

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa(TANAPA), imesema iwapo watanzania hususani wanaoishi karibu na hifadhi za taifa na mbuga za wanyama hawatakuwa walinzi wa rasilimali za taifa, upo uwezekano wa wanyama kama mbwa mwitu, tembo, sokwe na faru mweusi wakatoweka.

Kutokana na hali hiyo, huenda wanyama hao wakaonekana zaidi kupitia picha za video na za mnato, na kutaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa rasilimali hizo kwa kuwataja majangili wanaojihusisha na uwindaji harama wa wanyama hao.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kijazi amesema hayo wakati akifungua warsha ya siku tatu ya waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro, iliyoandaliwa na chama cha wanahabari mkoani hapa (Mecki) na kuratibiwa na hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA) na kufanyika mjini Moshi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu, Mkurugenzi wa uhifadhi wa Tanapa, Mtango Mtahiko, amesema Tanzania ni moja ya nchi zenye sifa ya uhifadhi wenye uoto wa asili jambo ambalo limekuwa likivuta idadi kubwa ya watalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu