Usain Bolt anaamini kuwa klabu yake pendwa ya Manchester United, ndio itakayoibuka na Ubigwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu huu.
Man United inayonolewa na kocha Jose Mourinho, ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 9, baada ya kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mpaka sasa.
Bolt ambaye ni mshindi mara nane wa medali za dhahabu aliyestaafu riadha mwaka huu, alionekana akiwa jukwaani akishuhudia mchezo baina ya Man Utd na Leicester City, ambapo Man Utd waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Bolt anaamini United ndio watakao shinda ubigwa wa ligi kuu msimu huu tangu walipofanya hivyo mwaka 2013.
