SERIKALI IMESEMA IMEANZA KUANDAA UTARATIBU WA KUUBORESHA MJI WA DODOMA, IKIWEMO KUZIPITIA SHERIA MBALIMBALI ZILIZOUNDA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU( CDA), KWA LENGO LA KUZIFANYIA MAPITIO NA KUZIBORESHA.
HAYO YAMEBAINISHWA BUNGENI MJINI DODOMA NA WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH,KASSIM MAJALIWA ,WAKATI AKIJIBU SWALI LA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA DODOMA MH,KUNTI MAJALA ALIYETAKA KUJUA NI LINI SERIKALI ITATEKELEZA AHADI YA KUIFUTA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU(CDA), KAMA ILIVYOTOLEWA NA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI ,WAKATI AKIOMBA RIDHAA KWA WANANCHI WA MANISPAA YA DODOMA KIPINDI CHA KAMPENI.
WAZIRI MKUU AMESEMA SHERIA ILIYOPO SASA IMEIPA CDA MAMLAKA PEKEE YA KUMILIKI ARDHI,HIVYO HIVYO KULETA WAWEKEZAJI NI LAZIMA KUIFUTA MAMLAKA HIYO.
