Uturuki yawakamata mameya wa chama cha upinzani.

Mamlaka za Uturuki leo zimewakamata na kuwavua madaraka mameya watano kutoka chama cha HDP kinachoiunga mkono jamii ya wachache ya wakurdi nchini humo.

Shirika la Habari la Uturuki, Anadolu, limeripoti kuwa mameya wa miji miwili na wilaya tatu wanazuiliwa kwenye makaazi yao kama sehemu ya uchunguzi unaohusiana na ugaidi.

Duru za habari pia zimearifu kuwa polisi ya Uturuki ilifanya upekuzi chini ya ulinzi mkali kwenye majengo ya manispaa.

Serikali ya Rais Reccep Tayyip Erdogan inadai kuwa chama cha HDP kina mafungamano na chama cha wakurdi kilichopigwa mafuruku cha PKK ambacho kwa miongo kadhaa kinaendesha uasi dhidi ya serikali ya Uturuki.

Licha ya HDP kupinga madai hayo, hadi sasa jumla ya mameya 45 wa chama hicho wameondolewa madarakani tangu kumalizika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo mwezi Machi 2019.

Exit mobile version