Uundwaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA wampa matumaini Rais wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, ameeleza matumaini ya kuundwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA na kuanza kazi zake vyema.

Dk Shein ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar,alipokutana na uongozi wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira, pamoja na Bodi ya Wakurugenzi ya ZURA na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA.

Dk Shein amesema ZURA imeweza kuleta matumaini makubwa katika kutatua changamoto zilizokuwapo siku za nyuma, katika suala la uhaba na upandishaji wa bei ya mafuta kiholela, uliokuwa ukitokea na kuleta usumbufu kwa wananchi.

Dk Shein amesema wananchi wanapaswa kuijua na kuitambua ZURA na kazi zake, ili kupeleka malalamiko yao hasa katika suala la bei ya mafuta.

Exit mobile version