UWEKAJI JIWE LA MSINGI KATIKA KITUO CHA AFYA ULENJE

In Kitaifa

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Benno Malisa ameweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya ulenje kilichopo katika halmashauri ya mbeya vijijini ambapo kituo hicho kinaendelea kujengwa kwa nguvu za wana nchi ujenzi huo uliaza Agost 2022 ambapo hadi sasa ujenzi umefikia hatua ya Renta ambapo wananchi hao wameiomba serikali kuwaunga mkono katika umaliziaji wa kituo hicho

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amechangia fedha Shilingi Million moja kwa wananchi wa Kata ya Ulenje kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa kituo cha afya ili kusaidia kuboresha huduma za afya huku mkuu wa Wilaya ya Mbeya kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Juma Homera amesema pamoja na mchango huo, Homera atahakikisha anafikisha kilio na ombi la wana Ulenje kuhusu umaliziaji wa ujenzi wa kituo hicho na upatikanaji wa hiduma bora katika kituo cha afya ulenje kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Diwani wa Kata ya Ulenje Mhandisi Boniface Njombe amesema kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya wananchi wake walianza ujenzi wa Kituo cha afya kwa kujenga majengo mbalimbali kuanzia Agosti 2022 ikiwemo kujenga jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, mapokezi na jengo la wagonjwa wa nje na wamefikia hatua ya Renta na kuwashukuru wadau walioshirikiana nao pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Oran Njeza.

Mbunge wa Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza amewapongeza wananchi wake wa Kata ya Ulenje kwa kuungana kujenga kituo cha afya na kuahidi kuendelea kuikumbusha Serikali kuwaunga mkono huku naye akichangia tena Shilingi milioni mbili

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akimwakikisha mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Z. Homera kwenye uwekaji jiwe la msingi ujenzi huo, amesema atahakikisha anafikisha kilio na ombi la wana Ulenje kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan la kuungwa mkono kwenye umaliziaji ujenzi huo unaohitaji fedha zaidi ya Sh. Million 400.

Pia ameahidi ofisi ya mkuu wa mkoa kuchangia fedha sh.milion moja na ofisi yake mkuu wa wilaya kuchangia shilingi laki tano ili kuwaunga mkono wananchi.

Wananchi wa kata ya Ulenje wanasema wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma za afya za uhakika maeneo ya mbali hata kulazimika kujifungulia njiani hivyo kujengwa kwa kituo hicho kutakuwa mkombozi hasa katika huduma za uzazi na mtoto.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu