Wakati utekelezaji wa makubalino baina ya Serikali na Barrick ukisubiriwa, Ofisa Mtendaji Mkuu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Acacia wametangaza kujiuzulu kuanzia leo Alhamisi.
Kwenye barua yake Ofisa Mtendaji Mkuu Bwana Brad Gordon amesema kuwa,anataka kurudi nyumbani Australia kusimamia masuala ya familia yake.
Wakati Ofisa Mkuu wa Fedha Andrew Wray akisema kuwa, yeye amepata fursa nzuri zaidi sehemu nyingine.
Pamoja na uamuzi huo wote wanaendelea kuhudumu kwenye nafasi hizo, wakati wakikabidhi majukumu ya ofisi kwa warithi wao, imesema taarifa ya Acacia iliyotolewa leo Alhamisi asubuhi.
Oktoba 20 Andrew aliwaambia waandishi wa habari kwamba, Acacia haina uwezo wa kulipa kiasi hicho kwa mkupuo
