Zaidi ya wananchi 420 mkoa wa Arusha wamenufaika na mafunzo ya
ujasiriamali pamoja na utengenezaji wa mitambo ya biogas kwa lengo la
kuachana na utumiaji wa nishata ya mkaa inayoharibu mazingira.
Aidha imeelezwa kuwa Tanzania ni kati ya nchi pekee katika jumuiya ya
Afrika mashariki inayotoa ruzuku kwa wananchi wake kuendeleza ujuzi na
stadi za maisha.
Akifunga mafunzo hayo kwenye kituo cha Gongal Model kilichopo eneo la
Njiro jijini Arusha na eneo la Gongali wilayani Karatu mwishoni mwa
wiki iliyopita Makam mkuu wa chuo cha Nelson Mandela amesema kuwa
mafunzo hayo yamekuwa ni mkombozi wa vijana kuondoka na changamoto za
ajira hivyo kuwataka vijana hao kuchangamkia fursa ya mafunzo hayo.
Amempongeza mtekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za mfuko
wa maendeleo ya elimu nchini TEA Dkt. Askwar Hilonga ambaye pia ni
mhadhiri wa chuo kikuu cha Nelson Mandela kwa kubuni na kuratibu wazo
hilo la kuokoa na kuhifadhi mazingira ya nchi yetu kwani takwimu na
maoni ya Rais Dkt.John Magufuli yanaonyesha zaidi ya kilimoeta 400
elfu zinaharibiwa kwa kuzalisha nishati ya mkaa.
Amesema mafunzo hayo yamekuwa na tija kwa vijana kuandaa mradi huo wa
kutengeneza Biogas na wao wataendelea kusaidia kuanzisha mtambo wa
kuzalisha funza ndani ya jiji la Arusha kwa mfano kwa lengo la kutumia
taka zinazozalishwa ndani ya jiji hilo.
Awali Mratibu wa mradi huo Dkt.Askwari Hilonga alisema kuwa vijana
waliomaliza wamekuwa wakipewa ofisi zao katika chuo hicho kwa lengo la
kuwasaidia kuendeleza taaluma walioipata katika mafunzo hayo.
Nae Mkurugenzi wa Miradi wa Tea Waziri Mouris amesema taasisi yao
itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kusaidia
utunzaji wa mazingira na taaluma hiyo wanampango wa kuianzisha kwenye
mashule ya sekondari nchini kuokoa utumiaji wa kuni na kuendelea
kutunza mazingira.
Akawataka vijana hao kutambua kuwa eleimu walioipata isiishie katika
kupata vyeti pekee bali wajikite kuanzisha viwanda vyao na kuandaa
maandiko yatakayosaidia kupata mikopo ya kukuza mitaji yao kwani ujuzi
wenu ndio mtaji sido wapo watawasaidia kufikia malengo yenu.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Camartec Paythias Ntella akieleza
umuhimu wa mitambo hiyo anasema kuwa inasaidia kuokoa uharibifu wa
mazingira nchini na kuacha matumizi ya nishati ya mkaa ambayo
inaharibu mazingira.
Hata hivyo mafunzo hayo yaliodumu kwa kipindi cha siku 30
yamewakutanisha wananchi wa maeneo mbali mbali mkoani hapa ambapo
imeelezwa kuwa ukiwa na Ng’ombe wapatao wawili unaweza kutengeneza
mtambo wa biogas na kuweza kuzalisha nishati ya gesi kwa matumizi ya
majumbani.
