Vijana sita wa timu ya Burundi ya ubunifu wa Maroboti watoweka.

Vijana sita wa timu ya Burundi ya ubunifu wa Maroboti wameripotiwa kutoweka baada ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa nchini Marekani.
Polisi imesema wawili kati ya vijana hao waliripotiwa kuonekana wakivuka mpaka wa Marekani kuingia Canada na kuongeza kuwa hakuna “dalili zozote za kutokea uhalifu”.
Hata hivyo Shirika la Huduma za Mpakani nchini Canada, limesema haliwezi kuthibitisha wala kukanusha kuwa vijana hao wawili waliingia Canada.
Wavulana hao wanne na wasichana wawili walionekana mara ya mwisho siku ya Jumanne mchana wakati mashindano hayo ya maroboti yalipokamilika mjini Washington.
Burundi kwa muda mrefu imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko, na kuongezeka kwa mapigano kumewalazimu watu  laki  nne ,kuyakimbia makazi yao tangu Aprili 2015, wakati Rais Pierre Nkurunziza aliposema atagombea muhula wa tatu.
Exit mobile version