Katika kuelekea katika uchaguzi mkuu Octoba mwaka huu, Viongozi mbalimbali Mkoani Singida wametakiwa kuachana na vitendo vya RUSHWA kwani ni kinyume cha utaratibu na hupelekea kupatikana viongozi wabovu.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa dawati la Elimu kwa Umma kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Singida Bw, Samsoni Julias wakati akitoa elimu ya RUSHWA kwa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi CCM UWT Mkoani humo.
Samson amesema hayo wakati Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida Bi Aisha Rose Matembe akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika wilaya ya Ikungi na Halmashauri ya wilaya ya Singida.
Afisa huyo wa TAKUKURU amesema kuanzia mwaka 2015 mapambano dhidi ya Rushwa yameanzia kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Amewasisitiza kuhakikisha wanakuwa makini ili kukwepa mkono wa Sheria kwa kujihusisha na RUSHWA hasa katika Kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.
