Viongozi wa Mamlaka ya hali ya hewa leo wametembelea ofisi za kituo cha Radio 5 Arusha na kujionea jinsi wanavyorusha matangazo yao.
Wakizungumza na baadhi ya watangazaji wa Radio 5, Bi Juwairia Mshana ambaye ni Meneja wa Mamlaka hiyo kanda ya Kaskazini amewashukuru Radio 5 kwa kuendelea kutoa taarifa za hali ya hewa katika vipindi vyao.
Kwa Upande wake Bw Charles Nsalamba ambae ni Meneja wa Mamlaka hiyo (TMA) mkoa wa Arusha amesema wadau mbalimbali wanapaswa kupata taarifa za hali ya hewa hivyo ni vyema kupata taarifa sahihi kutoka katika Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA).
Muwakilishi toka Uk Met ya nchini Uingereza ameipongeza Radio 5 kwa kuendelea kuwapa taarifa wananchi juu ya utabiri wa hali ya hewa.
Akizungumza mbele ya wageni hao kiongozi wa kipindi cha Kilimo Radio 5 Hilda Kinabo amewashukuru mamlaka hiyo kwa kuendelea kuwa karibu na Radio 5 hususani katika kutoa taarifa za hali ya hewa jambo linalo wasaidia kufikisha ujumbe kwa wakulima wanaotegemea Radio 5 kupata taarifa za hali ya hewa.
0
Kwa niaba ya Uongozi wa Radio 5 msimamizi wa vipindi wa kituo cha Radio 5 Bw Semio Sonyo amewashukuru viongozi wa TMA Mkoa na wa Kanda ya kaskazini pamoja na mgeni toka nchini Uingereza kwa kujali kile kinacho fanyika Radio 5 na kuwaomba waendelee kushirikiana na kituo chao katika kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi toka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania.
Radio 5 Arusha inarusha Matangazo ya hali ya hewa katika vipindi vyake kama Antenna,Fahari Yangu na vinginevyo.
