Viongozi wa Mashtaka nchini Uganda wanakutana leo kuamua ikiwa wasitishe mgomo.

Viongozi wa Mashtaka nchini Uganda wanakutana leo kuamua ikiwa wasitishe mgomo ambao umekuwa ukiendelea kwa karibu wiki moja sasa na kukwamisha kesi Mahakamani wakidai nyongeza ya mshahara.
Hatua hii inakuja baada ya serikali kuwaomba miezi mitatu kushughulikia madai yao na kuwaomba kurejea kazini ili kuepusha msongamano wa kesi mbalimbali nchini humo.
Majaji wamekuwa wakiashirisha kesi nchini Uganda kwa ukosefu wa viongozi hao wa Mashtaka.
Msemaji wa muungano wa Viongozi wa Mashtaka nchini humo Aliwali Kizito, ameiambia runinga ya NBS kuwa mkutano mkuu wa viongozi hao wa mashtaka ndio wanaoweza kusitsiha mgomo huo.
Mgomo huu umesababisha kucheleweshwa pia kwa kesi kuhusu mauaji ya aliyekuwa msemaji wa Polisi Andrew Felix Kaweesi.
Exit mobile version