Viongozi wawili wa upinzani nchini zimbabwe waunda umoja wao ili kuwania uchaguzi Mkuu ujao nchini humo.

In Kimataifa

Viongozi wawili wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuunda umoja kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Kiongozi wa Movement for Democratic, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Joice Mujuru wa National people’s Party walitia saini makubaliano hayo siku ya Jumatano.

Rais wa nchi hiyo Robert Mugabe awali alitoa maneno ya dhihaka kutokana na mipango ya upinzani aliyodai kuungana kumuondoa madarakani.
Morgan Tsvangirai na Joice Mujuru wameonekana kumaliza baadhi ya tofauti zao.Tsvangirai anasema makubaliano yaliyotiwa saini baina ya vyama viwili ni msingi kuelekea kuunda umoja wa vyama kwa ajili ya kupambana na chama tawala Zanu PF.
Changamoto iliyopo hivi sasa ni kuamua nani kati ya hao wawili ataongoza muungano huo.
Tayari, vyama vingi vidogo vya upinzani vimemuidhinisha Morgan Tsvangirai kuwa mgombea wao wa urais.
Kiongozi wa miaka mingi madarakani Robert Mugabe , alieleza kuwa upinzani umejaa watu wasio na kitu vichwani.
Amesema hakosi usingizi kwa kile kinachoitwa umoja wa wapinzani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu