Visa vipya 1,160 vya corona Afrika Kusini vyarekodi kwa siku moja.

Afrika Kusini imeripoti visa vipya 1,160 vya maambukizi ya virusi vya corona ambayo ni ya juu kabisa kuwahi kuripotiwa kwa siku moja tangu mwezi Machi ambapo kulirekodiwa kisa cha kwanza. Kulingana na taarifa iliyotolewa na wizara ya afya nchini humo, jimbo la Western Cape, maarufu kwa utalii limerekodi takriban asilimia 60 ya visa jumla nchini humo, vilivyofikia 15,515. Idadi ya vifo imeongezeka hadi 263, baada ya vifo vingine vitatu kuripotiwa kuanzia juzi, Jumamosi. Afrika Kusini ndiyo yenye idadi kubwa ya maambukizi barani Afrika ikifuatiwa na Misri yenye maambukizi 11,719 na vifo 612.

Exit mobile version