Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa vikicheza nyimbo za uhuru za kuanzia wakati wa uhuru miaka ya themanini na kurudia matangazo ya Meja Jenerali Sibusiso Moyo.
Jenerali Moyo alitangaza kupitia kituo cha runinga cha serikali nchini Zimbabwe (ZBC) TV kuwa jeshi lilikuwa limetwaa madaraka na kuwa Rais Robert Mugabe alikuwa salama.
Pia kituo cha radio cha serikali nacho kilitangaza taarifa hiyo ya Jenerali Moyo.
Vituo hivyo havijatangaza matangazo mengine.
Nyingi ya nyimbo hizo ni kuhusu vita vilivyoendeshwa na wapiganaji wa nchi hiyo dhidi ya utawala wa wazungu.
