Vyama ndugu vya kihafidhina vinavyomuunga mkono kansela wa Ujerumani vyaendelea kuwa na uongozi wa kutosha katika uchunguzi wa maoni ya wapiga kura.

Vyama ndugu vya kihafidhina vinavyomuunga mkono kansela wa Ujerumani Angela Merkel vinaendelea kuwa na uongozi wa kutosha katika uchunguzi wa maoni ya wapiga kura uliyochapishwa leo, chini ya miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Ulaya.
Chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha Social Democrats SPD, kilipata kupanda katika uungwaji mkono katika uchunguzi wa maoni baada ya chama hicho kumchagua spika wa zamani wa bunge la Ulaya Martin Schulz mwezi Januari kuongoza kampeni za chama hicho kumuondoa madarakani Merkel katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Septemba.
Lakini uchunguzi wa maoni ya wapiga kura kutoka mashirika ya INSA na Forsa unaelekeza kwamba kile kilichokuwa kinajulikana kama athari ya Schulz kimepungua wakati chama cha SPD kinaingia katika awamu ngumu ya kampeni kwa ajili ya uchaguzi mwezi ujao, mmoja kati ya chaguzi ndogo katika jimbo la kaskazini la Schleswig-Holtein, na mwingine katika jimbo la North Rhine Westphalia, jimbo lenye watu wengi zaidi nchini Ujerumani.
Uchunguzi huo unaonesha kwamba chama cha kansela Merkel cha CDU na CSU vitapata asilimia 36 wakati SPD itapata asilimia 30

Exit mobile version