Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeiandikia barua Ofisi ya Bunge vikipinga adhabu iliyotolewa juzi dhidi ya wabunge wawili wa umoja huo, Halima Mdee na Ester Bulaya.
Aidha umoja huo umeiomba ofisi hiyo kuitisha kikao cha Kamati ya Kanuni, ili ipitie na kutoa uamuzi juu ya upungufu inaodai kujitokeza katika kutoa adhabu dhidi ya wabunge hao.
Juzi Bunge liliazimia kupitisha hoja ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe Juliana Shonza CCM, kuwafungia kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge wabunge hao wawili kutokana na utovu wa nidhamu.
Jana hapakuwa na mbunge yeyote wa Chadema bungeni, kutokana na wengi wao kuhudhuria mazishi ya mwasisi wa chama hicho Phillemon Ndesamburo mkoani Kilimanjaro
