Waasi Nchini Ivory Coast wajeruhi watu sita katika mji wa Bouake.

In Kimataifa
Wanajeshi wanaoasi nchini Ivory Coast wamewajeruhi watu sita katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Bouake wakati huu wasiwasi ukiendelea kushuhudiwa nchini humo kuhusu hatima ya madai yao.
Imethibitishwa kuwa waliojeruhiwa  ni wanaume watano na mama mmoja mwenye watoto watatu.
Watu hao wanaendelea kupata matibabu hospitalini mjini Bouake na imeelezwa kuwa walipata majeruhi hayo baada ya risasi zilizokuwa zinafwatuliwa hewani,  kuingia ndani ya makaazi yao.
Ripoti zinasema kuwa watu wengine 15 walipata majeraha madogo na wanaendelea kupata matibabu.
Wanajeshi hao waliomsaidia rais Allasane Outtara kuingia madarakani mwaka 2010, siku ya Ijumaa walianza kuandamana na kuzingira makao makuu ya jeshi jijini Abidjan wakidai ahadi ya malipo yao kutoka kwa serikali.
Fofana, msemaji wa wanajeshi hao 8,400 alijtokeza na kusema kuwa wanajeshi hao wanaomba radhi na wameachana na mpango wao wa kuendelea kushinikiza kulipwa fedha zao.
Waasi hao wa zamani wanadai kulipwa Euro 18,000 kwa kile mwanajeshi, lakini wamefanikiwa kulipwa Euro 7,500 na ripoti zinasema kuwa ilikuwa imepangwa kuwa watapokea malipo mengine mwezi huu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu