Wabunge sita wa Chadema usiku wa kumkia leo wamehojiwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia Mbunge

In Kitaifa

Wabunge sita wa Chadema usiku wa kumkia leo wamehojiwa na polisi kwa tuhuma za kumshambulia Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza.

Mwenyekiti mwenza wa wabunge wanaounda umoja wa katiba (Ukawa) James Mbatia amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Mbunge wa Mlimba Suzan Kiwanga, Saed Kubenea(Ubungo), Pauline Gekul (Babati Mjini), Frank Mwakajoka (Tunduma), Joseph Selasini (Rombo) na Cecilia Pareso (Viti Maalum).

Hadi saa 5.00 usiku wabunge hao bado walikuwa wakiandika maelezo katika kituo cha polisi, Wabunge hao ni kati ya wabunge wanane waliotajwa na Spika wa Bunge Job Ndugai alipokuwa akiahirisha kikao cha bunge jioni kuwa wanatuhumiwa kumshambulia Shonza.

Wabunge wengine waliotajwa katika sakata hilo lililotokea Jana  mchana katika lango la kuingilia jengo la utawala ni Devotha Minja (Viti Maalum) na Cecil Mwambe (Ndanda).

Hata hivyo James Mbatia alipohojiwa Saa 5.45usiku alisema kuwa wabunge hao waliachiwa kwa dhamana baada ya mahojiano na kutakiwa kurud polisi leo  Saa 3 asubuhi.

Hata hivyo Mbatia ameshangazwa na kitendo cha kutajwa kwa Mwambe ambaye amesema hii ni wiki ya pili hayupo mjini Dodoma.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu