Wabunge wa UKAWA wasusia Bunge.

In Kitaifa, Siasa

Wabunge wa Upinzania Bungeni wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA waligoma kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge wakati Wabunge 8 wapya wa Viti Maalumu wa CUF wakiapishwa kuchukua nafasi ya Wabunge waliofutwa CUF.

Wabunge hao wamegoma kuapishwa kwa Wabunge hao wapya wakisema kuwa hawakubaliani na hatua hiyo, kwa kuwa haijafuata misingi ya kisheria na wanawaunga mkono wenzao waliofukuzwa.

Antena imenasa sauti ya Mbunge wa Momba Mh David Ernest Linde na hapa anaelezea kuhusiana na wao kugoma kuingia ndani ya Bunge wakati wenzao wanaapishwa.

Tayari wabunge hao wamehapishwa lakini Mh David Ernest ambaye ni katibu wa kambi rasmi Bungeni amesema kuwa, hawatowapa ushirikiano wabunge hao mpaka kesi ya msingi itapokwisha mahakamani.

Na kwa upande wa katibu wa bunge wa CUF MhJuma Hamad, yeye amesema hawakufurahishwa na mchakatako mzima wa kufukuzwa kwa wabunge, ndani ya chama chenye mgogoro  haikufata misingi ya katiba na sheria.

Wabunge ambao wamekula kiapo cha uaminifu leo ni pamoja na  Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim, Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.

 

Baada ya kula kiapo hicho cha uaminifu, Spika wa Bunge Job Ndugai akawa na neno kwa wabunge hao na wabunge wengine katika bunge hilo.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

NACTIVET YASIMAMISHA MAFUNZO CHUO CHA MBEYA TRAINING..DC MALISA AAGIZA KUFANYIWA UHAKIKI VYUO VYOTE WILAYA YA MBEYA

Wazazi Wanafunzi na wahitimu wa chuo cha Mbeya training wameiomba serikali iwasaidie kurudishiwa stahiki zao mara baada ya kubainika

Read More...

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE NOVEMBA 7, 2023

Manchester United na Newcastle United zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 20, ambaye mkataba wake unamalizika Juni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu