Wabunge wa Upinzania Bungeni wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA waligoma kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge wakati Wabunge 8 wapya wa Viti Maalumu wa CUF wakiapishwa kuchukua nafasi ya Wabunge waliofutwa CUF.
Wabunge hao wamegoma kuapishwa kwa Wabunge hao wapya wakisema kuwa hawakubaliani na hatua hiyo, kwa kuwa haijafuata misingi ya kisheria na wanawaunga mkono wenzao waliofukuzwa.
Antena imenasa sauti ya Mbunge wa Momba Mh David Ernest Linde na hapa anaelezea kuhusiana na wao kugoma kuingia ndani ya Bunge wakati wenzao wanaapishwa.
Baada ya kula kiapo hicho cha uaminifu, Spika wa Bunge Job Ndugai akawa na neno kwa wabunge hao na wabunge wengine katika bunge hilo.