Wachezaji wa Marekani wakamatwa kwa wizi China.

In Kimataifa, Michezo

wachezaji watatu wa mpira wa vikapu wa ligi ya vyuo nchini Marekani wamekamatwa nchini China kwa wizi wa dukani kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Wachezaji hao wa chuo kikuu cha California, mjini Los Angeles UCLA walikamatwa katika duka la Louis Vuitton kulingana na chombo cha habari cha ESPN.

Klabu hiyo ya UCLA iko nchini China kushiriki katika mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya timu nyengine ya Marekani Georgia Tech.

Watatu hao walikamatwa siku ya Jumanne , siku moja kabla ya ziara ya rais Donald Trump nchini China.

Wachezaji wanaozuiliwa katika mji wa Hangzhou ni Cody Riley, LiAngelo Ball na Jalen Hill kulingana na gazeti la Los Angeles Times na ESPN ikitaja duru ambazo hazikutajwa.

”Tunaelewa kuhusu hali iliowapata wachezaji wa UCLA mjini Hangzhou, China”, alisema msemaji wa klabu hiyo Shana Wilson katika taarifa yake kwa vyombo vya habari vya Marekani.

”Chuo hicho kinashirikiana kikamilifu na mamlaka husika kuhusu swala hilo na hatuna maelezo zaidi wakati huu”.

Wanafunzi watatu wa Georgia pia walihojiwa lakini hawakukamatwa , Chuo hicho kilisema kwa vyombo hivyo vya habari.

Klabu hizo mbili ziko China ikiwa ni miongoni mwa malengo yao ya Pac-12 Global initiative ya kupija jeki uwepo wao na uzoefu wa kibinafsi wa wachezaji.

Mechi hiyo ya kufungua msimu siku ya Ijumaa mjini Shanghai inafadhiliwa na Alibaba.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu