Mara baada ya wakala wa huduma ya ununuzi serikalini GIPSA kuanzisha mfumo mpya wa ununuzi katika mtandao ujulikanao kama TANEPS baadhi ya wafanyabiashara jijini Arusha wameanza kujitokeza na kujiunga na mfumo huo ili kuweza kurahisisha kazi zao na kuepukana na gharama
Akizungumza na vyombo vya habari meneja wa wakala wa huduma ya ununuzi mkoani Arusha Mihani Mihambo amesema kuwa mfumo huo ulikuja ili kuweza kuwarahisishia wafanyabiashara na makampuni binafsi kazi zao na kuendana na sayandi na technologia
Amesema kuwa mfumo huu umekuja chini ya sheria no 30 ya wakala wa GIPSA ambayo imeanza kutekelezwa kwa kupitia ununuzi wa pamoja wa vifaa na huduma mtambuka ambapo zabuni hizo zimeshatangazwa kwa mfumo hio wa kisasa
Amewataka wananchi kujisajili mapema ili kuweza kuokoa muda na kuepukana na usumbufu na badala yake waweze kufika kwenye ofisi husika ili kuweza kukamilisha usajili huo
Hata hivyo GIPSA ni wakala wa serikali, ambao majukumu yake, kutoa huduma za ununuzi wa vifaa na huduma mtambuka katika serikali
