Wafanyakazi wa Hotel ya seventy seven walipwa mafao yao.

In Kitaifa

Wizara ya Fedha na Mipango imesema kuwa waliokuwa wafanyakazi  wa Hoteli ya Seventy Seven ya mkoani Arusha, walioachishwa kazi mwaka 2000, wameshalipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria na taratibu hivyo  hawastahili kudai malipo yoyote ya nyongeza.

Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango (MB), Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maaluum (CCM) Arusha, Mhe. Catherine Magige aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa mafao waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo.

Mhe. Magige aliliambia Bunge kuwa waliokuwa wafanyakazi wa hoteli hiyo ambao waliachishwa kazi mwaka 2000, hawajalipwa mafao yao hadi sasa.

Akijibu swali hilo, Dkt. Kijaji amesema kuwa katika zoezi la ulipaji wa mafao kwa wafanyakazi hao Serikali ililipa Sh. Mil 217,366,296 mwezi Januari, 2000 ambapo baadae walipokea malalamiko kutoka kwa wafanyakazi hao kuwa wamepunjwa.

Hata hivyo, Mhe. Magige hakuridhishwa na majibu ya Dkt. Kijaji na alipopewa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza alisema kuwa Serikali imewalipa wafanyakazi hao awamu ya kwanza tu na hawakupewa nyongeza yoyote licha ya kuwasilisha malalamiko hayo.

Mhe. Magige aliongeza kuwa Wizara ya Fedha ilishawahi kwenda kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu, na Serikali iliipa jukumu la kusimamia malipo hayo Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo mpaka sasa bado haijalipa.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (MB), Mhe. Ramo Makani aliliomba Bunge limpe muda wa kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu ili aweze kutoa majibu sahihi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu