Waziri mku wa Iraq Haider al-Abadi ameamrisha wafanyakaziwote wa serikali kuchukua likizo leo Alhamis kutokana na kuwepo viwango vya juu zaidi vya joto.
Watabiri wa hali ya hewa wanatarajia viwango vya joto kwenye mji mkuu Baghdad kufikia nyuzi 50C leo alasiri
Jito jingi pia linatarajiwa miji ya Basra na Mosul,Joto hilo jingi linaweza kusababisha ukosefu wa nguvu za umeme.
Viwango vya juu vya joto vinashuhudiwa kote eneo hilo na tayari vimeathiri maeneo ya bara la Ulaya siku za hivi karibuni.
Wanasayansi wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha vifo vya watu Elfu hamsini na mbili barani Ulaya mwaka 2100.
