Wafuasi 12 wa CHADEMA wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo Maromboso leo tarehe 6.11.2017 na kusomewa makosa mawili, kosa la kwanza ni kufanya fujo ambapo inadaiwa walimfanyia fujo ndugu Juma Jumanne.
Kosa la pili shambulio la kawaida ambapo inadiwa walimshambulia mlalamikaji kwa kumpiga ngumi na sehemu mbalimbali za mwili.
Hakimu Obadia Mathias Mongi wa Mahakama ya Mwanzo Maromboso alisema Dhamana ya wafuasi hao ipo wazi kwa sharti lakuwa na wadhamini wawili na ahadi ya shilingi laki sita kwa kila mmoja.
Washtakiwa wote wametimiza sharti la dhamana
Washtakiwa wote wametakiwa kufika Mahakamani tena siku ya Alhamisi tarehe16.11.2017.
