Wafungwa 35 wauawa Gerezani.

 

Gavana wa jimbo la Amazonas nchini Venezuela, amesema zaidi ya wafungwa 35 wameuawa katika kile kilichoitwa mauaji ndani ya gereza.

Kikosi maalumu cha jeshi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo, kimepelekwa kudhibiti hali ndani ya gereza katika mji mkuu wa jimbo hilo Puerto Ayacucho.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa, walisikia milio ya risasi kwa saa kadhaa ndani ya gereza hilo.

Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali mpaka sasa,juu ya vifo vya wafungwa hao.

 

Exit mobile version