Waganga wakuu kupewa mikataba mwezi septemba.

Serikali inatarajia kutoa mikataba ya uwajibikaji kwa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini ifikapo mwezi ujao.

Imeeleza kuwa mikataba hiyo itadhibiti wale wanaojikita zaidi katika hospitali binafsi, kwa ajili ya kutafuta kipato cha ziada.

Kwa mujibu wa mikataba hiyo daktari atakayeshindwa kufikia malengo, atakuwa amejiachisha kazi mwenyewe.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Dk Zainabu Chaula, amesema lengo la mikataba hiyo ni kuboresha huduma za afya kwa kuwa haziridhishi.

Exit mobile version