Wageni wa La Liga waishangaza Real Madrid.

In Kimataifa, Michezo

Klabu ya Ginora ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Municipal de Montilivi, iliwaangushia kipigo cha mabao 2-1 Real Madrid katika mchezo wa ligi kuu ya Hispania La Liga uliopigwa jana.

Real Madrid walitangulia kufunga bao la kuongoza lililofungwa na Isco dakika ya 12 kipindi cha kwanza, lakini Ginora ambao ni wageni wa La Liga walitoka nyuma na kusawazisha bao hilo kipindi cha pili dakika ya 54 kupitia kwa Cristhian Stuani.

Wakati Madrid wakiwa hawaamini kilichotokea dakika ya 58, Portu struck aliifungia Ginora bao la pili na kufanya mchezo huo kumalizika kwa Ginora kushinda mabao 2-1.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana katika La Liga, na wamejiwekea historia kwa kuwapiga Real Madrid ambao ni mabigwa watetezi wa La Liga.

Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kushuka mpaka nafasi ya 3 ikiwa imecheza michezo 10 na kuvuna pointi 20, nyuma ya Valencia yenye pointi 24 na Barcelona ambao wapo kileleni wakiwa na pointi 28.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu