wagombea wawili wa upinzani kupambana na rais Paul Kagame wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.

In Kimataifa
Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda, imewaidhinisha wagombea wawili wa upinzani kupambana na rais Paul Kagame wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi ujao.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Profesa Kalisa Mbanda amesema wanasiasa hao wawili wa upinzani waliokidhi vigezo vya kuwania urais ni pamoja na Frank Habineza, kutoka chama cha Democratic Green Party na mgombea binafsi Philippe Mpayimana.
Gilbert Mwenedata, Fred Barafinda Skikubo na mwanamke wa pekee Diane Rwigara, hawakufanikwia kuidhinishwa baada ya kukosa kupata saini za wapiga kura 600 kama inavyotakiwa kikatiba.
Tume hiyo mwezi uliopita, iliwapa siku tano wagombea hao kuhakikisha kuwa wanatimiza vigezo hivyo la sivyo wafungiwe kushiriki katika Uchaguzi huo.
Kigezo ambacho hawakutimiza ni kutopata sahihi za wapiga kura 600 kutoka kwa wilaya 12 kati ya 30 nchini humo.
Wagombea binafsi wamekuwa wakilalamikia kusumbuliwa na maafisa wa usalama katika harakati zao za kujitambulisha kwa raia wa nchi hiyo na kueleza mipango yao.
Kampeni zinatarajiwa kuanza katikati ya mwezi huu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu