Wagombea wawili waenguliwa Meru Nassari akata rufaa.

Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari amekata rufaa kupinga hatua ya kuenguliwa kwa wagombea wake wawili waliopitishwa kugombea udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa marudio unaofanyika katika kata tan0 Jimbo la Arumeru Mashariki.

Mwanasheria wa CHADEMA anayesimamamia mapingamizi hayo Shedrack Mfinanga amethibitisha kuandika barua ya malalamiko kwa tume ya uchaguzi kupitia kwa msimamizi wa uchaguzi mdogo wa madiwani katika halmashauri ya Meru Ramadhani Madili.

Amesema msimamizi huyo wa uchaguzi ana sifa ya kuwaengua wagombea udiwani sio kazi yake na alipaswa kupeleka mapendekezo yake kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ili aweze kuyatolea uamuzi.

Exit mobile version