Wagonjwa wa akili waongezeka Tanzania.

 

 

Tafiti zilizotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zinaonyesha kuwa, magonjwa ya akili yameongezeka kutoka wagonjwa laki 6 mwaka 2014-2015, hadi kufikia wagonjwa laki 7 kwa mwaka 2015-2016.

Takwimu hizo zimetolewa na Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Magonjwa yasiyopewa kipaumbele, katika wizara ya afya nchini Bw Shadrack Buswelu kwenye mafunzo kwa watumishi wa magereza na hospitali za mikoa.

Amesema kinachochangia ongezeko la ugonjwa wa akili kuongezeka nchini, ni mfumo wa maisha ulivyo kwa sasa, magonjwa sugu na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake Mratibu wa Magereza SP Wambili Bwatai, amesema tatizo la magonjwa ya akili gerezani ni mara mbili ya wagonjwa waliopo nje.

 

Exit mobile version