Wagonjwa wa Corona nchini Kenya Wamefika 737 baada ya wagonjwa wapya 22 kuripotiwa ndani ya masaa 24 yaliyopita.
Idadi hiyo ni kati ya sampuli 1,516 zilizopimwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Amesema kwamba kufikia sasa serikali ya kenya imefanikiwa kuwapima watu 35, 432 .
21 kati ya wagonjwa hao ni Wakenya huku mmoja akiwa raia wa Uganda.
Katika mkutano wake na wanahabari katibu tawala wa waziri wa Afya Rashid Aman amesema kwamba wagonjwa wanne wamefariki kutokana na virusi hivyo, watatu kutoka Nairobi na mmoja kutoka Mombasa.
Hatua hiyo inaongeza idadi ya waliofariki kutokana na Covid-19 kufikia watu 40.
