Wagonjwa wa corona wagundulika kwenye kambi za warohingya.

Wafanyakazi wa afya leo wameanza juhudi za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona kwenye kambi inayowahifadhi karibu wakimbizi milioni 1 wa jamii ya wachache ya waislamu wa Rohingya baada ya kurikodiwa kisa cha kwanza cha virusi hivyo Mtu mmoja kutoka jamii ya wakimbizi hao na mkaazi mwingine wa wilaya ya Cox´s Bazar iliyopo kusini ya Bangladesh wamegundulika kuwa na virusi vya corona na tayari wametengwa.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi amesema watoa huduma za afya tayari wameanza kuwahudumia wagonjwa hao wawili, pamoja na kuwafuatilia wote waliokutana nao kwa lengo la kuwaweka karantini.

Kwa muda mrefu kumekuwa na wasiwasi kwamba virusi vya corona vitasambaa kwa kasi iwapo vitaingia katika kambi 34 zinazowahifadhi wakimbizi wa Rohingya kutokana na hali duni ya miundumbinu kwenye maeneo hayo.

Exit mobile version