Wakati Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha, Innocent Mushi na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana wakipandishwa kizimbani kutokana na vifo vya watu 35 wakiwemo wanafunzi 32 wa shule hiyo, ndege maalumu inatarajiwa kutua nchini leo kuwabeba majeruhi watatu wakatibiwe Marekani.

WAKATI Mkurugenzi wa Shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha, Innocent Mushi na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana wakipandishwa kizimbani kutokana na vifo vya watu 35 wakiwemo wanafunzi 32 wa shule hiyo, ndege maalumu inatarajiwa kutua nchini leo kuwabeba majeruhi watatu wakatibiwe Marekani.

Mwinjilisti maarufu duniani kutoka Shirika la Samaritan Purse, Bill Graham wa Marekani na ndiye aliyebeba gharama za kukodisha ndege maalumu aina ya DC 8, kupeleka wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita wilayani Karatu, Arusha.

Watoto hao wanamajeraha  shingoni, miguu na sehemu mbalimbali za miili yao,Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu aliyezungumza jana na waandishi wa habari mjini Arusha, gharama za kukodisha ndege kwenda Marekani si chini ya dola za Kimarekani laki tatu 350,000 sawa na shilingi  (Sh milioni 700).

Gharama hizo ni nje ya matibabu, chakula na malazi kwa wakati wote ambao wagonjwa hao na

Aidha  ametumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kupongeza juhudi za Rais, Dk John Magufuli, Makamu wake, Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Mkoa wa Arusha chini ya Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo kwa kuguswa na kushiriki katika kila hatua kuanzia baada ya ajali, mazishi hadi ufuatiliaji wa afya za majeruhi.

Exit mobile version