WAKAZI WA ARUSHA WAHIZWA KUTUNZA AMANI YA JIJI LA ARUSHA AMBALO NI KITOVU CHA UTALII NCHI

In Kitaifa

Na. Abel Paul wa Jeshi la Polisi

Wananchi wa jiji la Arusha wamehimizwa kutunza amani na utilivu wa jiji hilo ambalo Lina sifa ya kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya Nchi ikiwa ni sifa ya kuwa na amani na utulivu miongoni mwa majiji hapa Nchini.

Hayo yamesemwa leo na kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO wakati akitoa taarifa kwa wananchi kuelekea sikukuu ya Mwaka mpya 2023 ambapo amewataka wananchi wa mkoa huo kufuata maelekezo yanayotolewa na serikal na Jeshi hilo ili kulinda heshima ya jiji hilo hapa Nchini.

Kamanda Masejo pia amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la mvua nyingi katika Mkoa wa Arusha kitendo kilichopekea madhara kwa wananchi ambapo amewataka wananchi wa Mkoa huo kuchukua tahadhari.

Aidha ACP Masejo amebainisha kuwa katika mvua zinazoendelea kunyesha zimepekea madhara na kusabisha vifo vya watu watatu ikwemo kijana mmoja aitwaje Baraka mwenye umri wa miaka (17) mwanafunzi ambaye alichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023.

Katika tukio jingine kamanda Masejo amesema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wa nne kwa kosa la kuiba gari moja Aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili IT 3CD50343065 ambapo liliwekewa namba bandia za usajili wa Nchi jirani KDA 222H kwa lengo la kuuzwa jijini Arusha.

Ameongeza kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kubaini mtandao mzima.

Mwisho amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo ili kuendelea kuimarisha amani na utulivu katika Mkoa huo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu