WAKUU wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wameonywa kuacha kushindana wenyewe kwa wenyewe, na kuendeleza migongano badala isiyo na tija badala yake washirikiane kwa kuwa wanategemeana , katika kutekeleza Majukumu yao.
Onyo hilo lilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene mjini Dodoma jana wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi hao wa mikoa sita kutoka Kanda ya Ziwa.
Simbachawene amewataka wachukuliane hali, hisia, tabia na wavumiliane na kushirikiana ,badala ya kuonesheana ubabe na kila mmoja kujiona ana madaraka kuliko mwenzie.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mussa Iyombe amewataka viongozi hao kujifunza kwa bidii katika semina hiyo, kujua vizuri Majukumu yao na Mipaka ya kazi yao badala ya kukaa siku tano na kurudi watupu.
Mafunzo hayo yamewashirikisha viongozi kutoka mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Simiyu, Manyara na Geita,
